Simba wapanga kikosi kibabe mechi ya Mtibwa Sugar

Thursday May 16 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara leo Jumanne.

Kikosi cha Simba kilianza katika mechi ya Mtibwa Sugar wakiwa na beki mmoja tu mwenye asili ya kucheza kati.

Beki huyo ambaye alianza katika kikosi cha kwanza ni Yusuph Mlipili akianza na kiraka Erasto Nyoni.

Mbali ya Simba kuondoka kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza, ambalo lilifungwa na John Bocco.

Katika benchi la wachezaji wa akiba Simba walikuwa na viungo Said Ndemla, Mohammed Ibrahim, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin.

Wengine waliokuwepo ni kipa Deo Munishi, na washambuliaji Rashid Juma na Adam Salamba.

Kipindi cha pili, Cleotus Chama  aliweka wavuni bao dakika ya 47 huku na Emmanuel Okwi aliwekwa wavuni bao  mwisho baada ya mabeki wa Mtibwa Sugar kupoteana

Advertisement