Breaking News
 

Simba wana mzuka kinoma, wafikia hoteli ya maana Mtwara!

Friday September 14 2018

 

By Thobias Sebastian

Mtwara. Kikosi cha Simba leo Ijumaa jioni kitafanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara tayari kwa mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Ndanda FC lakini hiyo morali ya wachezaji usipime.

Simba watacheza na Ndanda katika uwanja huo ugenini huku wakiwa na rekodi ya kutopoteza mechi nane walizocheza na timu hiyo. 

Mwanaspoti ambayo imeweka kambi hapa Mtwara imeshuhudia nyota wa Simba wakiwa na morali ya hali ya juu kuhakikisha wanashinda katika mechi hiyo.

Nyota wa Simba wamedhamilia kuendeleza rekodi ya kutofungwa wakati Ndanda wakitaka kuvunja rekodi ya miaka hiyo minne.

Mratibu wa Simba Abbas Ally amesema kambi ipo kamili kila mchezaji yupo sawa na

wanaimani kubwa ya kupata ushindi.

"Wachezaji wote wapo kamili na kila mmoja yupo na morali ya juu kuhakikisha tunarudi na pointi tatu, " alisema Abbas.

Mwanaspoti ilishuhudia nyota wa kikosi hiko wakipata chai kwa pamoja huku wakiwa na morali ya hali ya juu kwa kuhamasishana.

Simba wamefikia katika hoteli ya Tiffany iliyo katikati ya mji wa Mtwara.

 

Advertisement