Simba wageukia mbinu

Monday June 1 2020

 

By THOBIAS SEBASTIAN

Kikosi cha Simba baada ya kufanya mazoezi ya nguvu kwa juma zima lililopita leo wamefanya mazoezi ya mbinu.

Mara baada ya kikosi hicho cha Simba kuwasili uwanjani walifanya mazoezi machache ya viungo na baada ya hapo walionekana kufanya mazoezi ya kuchezea mpira zaidi.

Aina ya mazoezi hayo ya yalikuwa ni jinsi ambavyo timu yao itakuwa inazuia kwa maana ya kukaba wapinzani ambao watakutana nao.

Walifanya mazoezi mengine ya mbinu jinsi ambavyo watashambulia kwa aina tofauti kwa maana ya kupitia pembeni na kati kati ya uwanja.

Mazoezi mengine ya mbinu ambayo walifanya ni kupiga mashuti ya mbali, pasi ndefu na fupi kuanzia nyuma mpaka kufika langoni mwa timu pinzani.

Baada ya hapo walimalizia kwa mazoezi ya kufungua nafasi (Open Spaces), kisha kumaliza  kwa kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

Advertisement

Advertisement