Simba kupiga kambi Mbeya

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba leo Jumatatu Julai 27, 2020 wameondoka kuelekea jijini Mbeya ambako watapiga kambi ya siku tatu kabla ya kuelekea mjini Sumbawanga kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Simba watacheza fainali hiyo Agosti 2, 2020 dhidi ya Namungo FC, mechi itakayopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga huku vigogo hao wakiunganisha ndege moja moja baada ya kutua Dar es Salaam na kubadilisha ndege ya kutoka Moshi kwenda Mbeya.

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu, ameiambia Mwanaspoti Online, kuwa kikosi chao kilirejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mechi za ligi kuu mjini Moshi ambako walicheza na Polisi Tanzania na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 kwenye Uwanja wa Ushirika.

"Hivi sasa ninavyoongea tupo kwenye Ndege tunaelekea Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu na Namungo,"

"Mbeya tunaenda na Ndege, lakini mara baada ya kufika Mbeya itaturalazimu tupande basi kuelekea Sumbawanga kwa kuwa hakuna usafiri wa ndege kule,"