Simba kibaruani leo

Mabingwa watetezi, Simba SC inashuka uwanjani leo kuivaa Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, Simba itahitaji ushindi ili kujirudisha katika nafasi nzuri za kutetea taji la Ligi Kuu.

Kocha Sven Vandebroeck alisema vijana wake wapo katika hali nzuri licha ya kuwa na kumbukumbu mbaya za kipigo cha ugenini.

Simba inashuka uwanjani ikiwa imeshuka hadi nafasi ya nne na ushindi pekee utairudisha nafasi ya tatu inayoshikiliwa na Biashara United yenye pointi 16.