Simba SC wabadilike

Dar es Salaam. Kipigo cha bao 1-0 ilichpata Simba dhidi ya Tanzania Prisons kimeibua maoni tofautu ya wadau, ambao wamedai kuwa tafsiri ya kikosi kipana imekosekana.

Yanga ililala ugenini katika mchezo uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Nelson Mandera, Sumbawanga, kitendo kilichoibua taharuki kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Simba iliwakosa Chris Mugalu, Meddie Kagere, John Bocco, Pascal Wawa na kiungo fundi, Clatous Chama kutokana na sababu tofauti.

Kocha na mchambuzi wa masuala ya soka nchini Mwalimu Kashasha alisem tafsiri ya kikosi kipana kwa Simba ni kama haipo kutokakan ankukosekana kwa nyota wachache kuwa tatizo kwenye mchezo huo.

“Unakosa wachezaji wanne na kila kitu kinabadilika, hii haileti maana sahihi ya kikosi kipana, kinatakiwa kuwa na uwiano (kikosi).

“Anayetoka na anayeingia wanatakiwa wasiwe na tofauti, kwa maana hiyo kunakuwa na balance (uwiano sawa) kikosini. Lakini kilichotokea kwa Simba kila mtu amekiona, hawakuwa katika kiwango ambacho kimezoeleka,” alisema Kashasha.

Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Emmanuel Gabriel alisema pamoja na kocha kuwa na wachezaji wa kikosi cha kwanza anatakiwa kuwapa nafasi wale wanakuwa nje ili kulinda viwango vyao.

“Si kama Said Ndemla, Ajibu na wengine ni wabaya, ila hawapati mechi nyingi. Kocha awe anawapa dakika chache za kupata muunganiko, ili ikitokea tatizo kama la majeruhi timu inacheza kwa ubora ule ule.

“Lakini bado Simba inafungwa mabao ya aina moja ya krosi, wanatakiwa kuliangalia hilo pia na kulitafutia dawa, kwani wanakwenda kimataifa, huko watalaumiana sana,” alisema Gabriel.