Simba, Yanga zapigwa kijembe

Muktasari:

Akizungumza katika mkutano wa sita wa bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Karia alisema anashangazwa kuona klabu hizo zikicheza katika uwanja ambao una mabango mengine ya kampuni za kubeti.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ni kama amezipiga vijembe klabu ya Simba na Yanga baaada ya kukubali kucheza katika uwanja wenye mabango ambayo hawadhamini klabu hizo.
Akizungumza katika mkutano wa sita wa bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Karia alisema anashangazwa kuona klabu hizo zikicheza katika uwanja ambao una mabango mengine ya kampuni za kubeti.
"Simba na Yanga mnapewa pesa na Sportpesa lakini mnacheza Taifa kuna mabango ya Betting za kampuni nyingine (Jina kapuni) lakini mmenyamaza, lakini Simba walikutana na kisanga hiki CAF na hawakutangaza Sportpesa kwa sababu kule mdhamini mkuu ni kampuni ya kubeti," alisema.
Karia alisema kama watashindwa kufanya jitihada za kuondoa mabango hayo ambayo Simba wakicheza mechi za CAF mabango hayo hutolewa basi watafute viwanja vingine.
Akizungumzia kuhusu timu ambazo zina kodi viwanja alisema anataka kuona mikataba husika itakayoonyesha kukodishwa kwao.
"Tutaangalia mikataba kwa viwanja vilivyokodiwa, lakini pia kwa wale wa mikoa ambayo viwanja vyao vimewekewa viulizo wanatakiwa wajipange kwelikweli," alisema.