Simba, Yanga kucheza Uhuru

Saturday January 13 2018

 

By DORIS MALIYAGA

MECHI za mzunguko wa 13 wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Mwadui FC pamoja na Simba dhidi ya Singida United, zitachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Michezo hiyo ambayo Yanga ndiyo wataanza kuwakaribisha Mwadui siku ya Jumatano saa 10:00, jioni wakati  Simba wao watacheza na Singida, Alhamisi saa 10: 00, jioni.
Mkurugenzi mtendaji  wa bodi ya ligi, Boniface Wambura,  ameuambia mtandao wa Mwanaspoti kuwa michezo hiyo yote itachezwa kwenye uwanja wa Uhuru.
"Mechi zote za mzunguko wa 13, Yanga na Mwadui na ule wa Simba dhidi ya Singida, itachezwa kwenye  Uwanja wa Uhuru kwa siku za Jumatano na Alhamisi,"anasema Wambura.
Kauli ya Wambura ni kuwatoa wasiwasi mashabiki wa soka ambao awali walikuwa hawafahamu kuwa mechi hizo zitachezwa wapi, wapo waliofikiri zitachezwa Uwanja wa Taifa, Chamazi pamoja na huo wa Uhuru.