Simba, Yanga kama kawa mwanangu!

Thursday September 13 2018

 

By Thomas Ng'itu

 Dar es Salaam. Wale waliosambaza 'uzushi' kuwa mechi ya wakongwe Simba na Yanga inayotarajiwa kuchezwa Septemba 30,  imeahirishwa basi ipo kama kawaida na viingilio vimeshatangazwa.

Mechi hiyo ambayo huteka hisia za wadau wengi wa soka kutokana na namna timu hizo mbili kuwa na ushindani pamoja na idadi kubwa ya mashabiki.

Viingilio vitakuwa hivi,  VIP A 30,000, VIP B 20, 000, viti vya Machungwa na Kijani 7,000.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wao, Clifford Ndimbo amesema, tiketi zitaanzwa kuuzwa mapema kuanzia Septemba 20.

" Mchezo wa Simba na Yanga upo kama kawaida na utachezwa siku iliyopangwa, mashabiki wajitokeze kwa wingi kwennda kushabikia timu zao," alisema Ndimbo.

Ndimbo aliongeza, katika mchezo huo wamezidisha ulinzi wa kutosha ili mashabiki waweze kuwa na amani muda wote wakiwa wanafuatilia mchezo huo.

 

Advertisement