video: Simba: Mabao 5-0 ya Misri, Taifa lazima yarudi

Muktasari:

Mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly ya Sudan utakuwa wa nne katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Simba imepngwa Kundi D pamoja AS Vita, JS Saoula na Al Ahly.

Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterans leo Jumamosi ili kujiandaa na mechi yao dhidi ya Al Ahly ya Misri itakayopigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Simba umetangaza bei ya kiingilio kwenye mchezo huo ambacho kinaanzia Sh. 2000 kwa jukwaa la mzunguko, VIP A Sh15,000, VIP B Sh10,000.

Uamuzi huo umelenga kupata idadi kubwa ya mashabiki watakaojitokeza uwanjani siku hiyo ili kuiunga mkono timu hiyo kwenye mechi hiyo ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

Awali jana Ijumaa, Mwenyekiti Bodi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ alisema,  "Tulishawahi kuwafunga Zamalek hapa. Tulishawahi kuwafunga Enyimba hapa lakini hilo halitowezekana kama hatutopata sapoti ya mashabiki.”

“Pamoja na kufanya vibaya kwenye mechi mbili zilizopita, naamini kama tukipata ushindi kwenye mechi zinazofuata, bado tuna nafasi ya kusonga mbele.”

“Tumekaa kama bodi ya klabu na kuamua kiingilio kwenye mchezo huo kiwe Shilingi 2000. Tunajua kuwa tunahitaji fedha lakini matokeo ni ya muhimu zaidi," alisema MO.