Simaro Lutumba afariki dunia leo

Muktasari:

Franco aliyefariki dunia Oktoba 12, 1987, Pepe Kalle, Papa Wemba, Mayaula Mayoni na Madilu System. Taarifa zaidi juu ya msiba huo zinaendelea kufuatiliwa na mtahabarishwa na MCL Digital.

MSHIRIKA mkubwa wa zamani wa Luambo Luanzo Makiadi 'Franco', Simaro Massiya Lutumba amefariki dunia asubuhi ya leo Jumamosi jijini Paris, Ufaransa. Gwiji huyo aliyekuwa mahiri kwa kucharaza gitaa la rhythm, kutunga na kuimba amefariki akiwa na miaka 81.

Kwa mujibu wa mwanae Salomon Lutumba, gwiji huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kabla ya kukumbwa na mauti akitoka kuadhimidha siku yske ya kuzsliw machi 19 mwaka huu.

Kifo cha mkongwe huyo aliyekuwa mshirika mkubwa wa Franco na Josky Kiambukuta katika bendi ya TP OK Jazz kimemfanya aungane na magwiji wengine wa DR Congo waliotangulia mbele ya haki akiwamo Franco aliyefariki dunia Oktoba 12, 1987, Pepe Kalle, Papa Wemba, Mayaula Mayoni na Madilu System.

Taarifa zaidi juu ya msiba huo zinaendelea kufuatiliwa na mtahabarishwa na MCL Digital.