Siku tano zampa mzuka Zana

Friday March 22 2019

 

By Thobias Sebastian

Mapumziko ya siku tano ambayo wamepewa wachezaji wa Simba yamempa mzuka beki wa Simba, Zana Coulibaly.
Coulibaly aliliambia mara baada ya kupewa mapumziko ya siku tano na kocha wao Patrick Aussems alirudi kwao.
Zana alisema hayo akiwa kwao nchini Bokinafaso kuwa amepata muda wa kupumzika na familia yake ambayo imempa motisha na atakaporudi atakuwa vizuri zaidi ya alivyondoka.
Zana alisema nimepata muda wa kupumzika na familia yangu nduvu jamaa na marafiki ambao niliondoka hapa kuja kujiunga na Simba bila kuwaaga.
"Nitakuwa hapa nyumbani mpaka mwisho wa wiki hii na kubwa nimepata muda wa kutosha kupumzika na kuongea hata na makocha wangu walionifundisha kabla ya kuja Tanzania," alisema.
"Nikirudi Tanzania natamani kupambana ndani ya Simba ili kupata nafasi ya kucheza ili kuisadia timu kufikisha malengo yake.
"Kuhusu kupangiwa na TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni timu nzuri na kubwa ambayo tumejipanga kushindana nayo," alisema Coulibaly.

Advertisement