Sikia hiki anachosema Try Again

Tuesday September 11 2018

 

By KHATIMU NAHEKA

SIMBA imefunga jana zoezi la kuchukua fomu katika kugombea nafasi za uongozi lakini jina moja kubwa lililokuwa linasubiriwa kwa hamu lichukue fomu limegoma kugombea na kuwashtua Wana Msimbazi.

Kaimu Rais wa sasa wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again ndiye aliyekuwa akitarajiwa awanie Uenyekiti wa Bodi, lakini mwenyewe ameamua kuchomoa akisema haoni sababu ya kufanya hivyo sasa kwa kutunza ubora wake kiuongozi. Try Again ameliambia Mwanaspoti kwamba amechukua uamuzi huo ikiwa ni kuepusha mgongano wa kimaslahi katika yale aliyoyafanya chini ya uongozi wake.

Bosi huyo mwenye msimamo mkali alifafanua akisema katika kipindi cha uongozi wake Simba ilipiga hatua kubwa kwa kupitisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na endapo angegombea angedhaniwa alijitengenezea njia ya kukaa madarakani.

Advertisement