Sikia bosi wa La Liga anavyomchana Ronaldo

Muktasari:

  • Tangu Ronaldo ameondoka Real Madrid msimu huu na kujiunga na Juventus, katika La Liga kumeshudia Real ikiwa imeanza vibaya zaidi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 kupita

MADRID, HISPANIA. Rais wa La Liga, Javier Tebas amesema Cristiano Ronaldo hajaacha pengo lolote kwenye soka la Hispania na kama kuna kitu wanakimisi basi ni makocha wawili, Pep Guardiola na Jose Mourinho.

Bosi huyo mkuu wa ligi, alisema kama kuna kitu ambacho angependa kukifanya basi ni kuwarudisha Mourinho na Guardiola kwenye ligi hiyo, lakini kwa Ronaldo kwanza amechelewa kuondoka, hana la kumfanya akumbukwe sana.

Ronaldo aliachana na La Liga kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kuhama Real Madrid na kwenda kujiunga na Juventus kwa ada ya Pauni 88 milioni.

Huko kwenye kikosi cha Real Madrid kunadaiwa kuwa na shida katika kufunga mabao, lakini kwa Tebas haoni kama Ronaldo ameacha pengo na hawawezi kummisi kwa kuondoka kwenye La Liga. Tebas alisema La Liga bado ina mastaa kibao wenye majina makubwa na kwamba Ronaldo angemshtua kama angeondoka miaka minne iliyopita.

“Tumefanya kazi kuifanya La Liga kuwa nembo yenye kadhi kubwa kuliko mchezaji yeyote na klabu yoyote. Miaka minne iliyopita kama angeondoka ningeishtuka, kwamba kwenye kiwango cha moja ya kumi basi ningempa tisa. Lakini, kwa sasa wasiwasi niliona, kwenye moja ya kumi, basi ni nne au tatu tu.”

Tebas alisema kitu ambacho kitaka ni kuwa na ligi yenye wachezaji wote bora na makocha wote bora, akiwataja Guardiola na Mourinho, ambao kwa sasa wapo kwenye Ligi Kuu England wakizinoa klabu mahasimu, Manchester City na Manchester United.