Sibomana awaondoa wasiwasi Yanga

WINGA wa kushoto wa Yanga Patrick Sibomana amesema wala hakuwa na wasiwasi baada ya kukosa penalti ya kwanza katika mchezo dhidi ya Township Rollers.

Winga huyo amesema baada ya kukosa penalti ya kwanza aliumia kwa kupoteza nafasoi nzuri kwa timu yake lakini haikumuondolea hali ya kujiamini.

Raia huyo wa Rwanda amesema Yanga ilipopata penalti ya pili alijua anaweza kufunga na kuomba kupiga na kisha akapata.

Amesema bado ana imani kwamba Yanga ina nafasi katika mchezo wa marudiano licha ya kuanza kwa sare nyumbani dhidi ya Rollers.

Amesema watajipanga kufanya vizuri zaidi kutokana tayari wameshajua ubora wa wapinzani wao katika mchezo huo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili mbele.

Aidha Sibomana amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwa karibu na timu yao hatua ambayo itazidi kuwaongezea morali ya kupambana.