Shoo ya Bogoss usiku wa kuamkia leo usipime

Saturday September 1 2018

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Bendi ya Bogoss Musica El Classico ‘wazee wa kuliamsha dude’ usiku wa kuamkia leo Jumamosi  ilifanya onyesho yake ndani ya Ukumbi wa The Jonz uliopo Magomeni Mwembe-Chai Jijini Dar.

Bendi hiyo tangu ilipozinduliwe Julai 28 mwaka huu imejizolea umarufu mkubwa kwa mashabiki kutokana na maonyesho yake hali inayoonekana kurudi kwa muziki wa dansi Tanzania.

Akizungumza na MCL Digital  Mkurugenzi wa bendi hiyo, Nyoshi El Saadat ‘Rais wa Milele’ amesema siri ya bendi hiyo kuwa kwenye ubora na kukusanya umati wa watu ni kutokana na kuwa na  safu mpya ya vijana katika bendi hiyo.

“Unajua usione bendi imekubalika hivi, nimeamua kuja kivingine kwa kuwachukua vijana ambao hawajawahi kupiga bendi ya aina yoyote, nikawafundisha mwaka mmoja hadi wameiva na ndio maana unaona wanafanya vizuri hivi.

“Pia damu changa ndio habari ya mujini sahizi, yaani hapo unapowaona wanakuimbia nyimbo za aina yoyote hata ukitaka bongo fleva ya kwa mtindo wa dansi utaipata Bogoss Musica,” alisema Nyoshi El Saadat.

Aidha Nyoshi amesema Bogoss Musica wananyimbo nyingi ambazo bado hawajazitoa, wanasubiri huu wimbo  wa ‘Mama wa Kambo’ unaotumia Rapu ya ‘tunaliamsha dude’ na watapata tabu sana mashabiki waendelee kuupokea zaidi ndio watakuja kuachia nyimbo zingine.

“Siyo kwamba tuna wimbo mmoja tu wa ‘mama wa Kambo’ Bogoss inanyimbo zaidi ya kumi na sita, ambazo tumezitengeneza ndani ya mwaka mmoja, ila nimeona haipendezi mashabiki kuwatolea nyimbo nyingi itakuwa tunawachanganya,” alisema Nyoshi

Nyoshi aliwataja vijana waliokuwa kwenye safu ya uimbaji kuwa ni pamoja na  abouador, Uncle Some, Dizzo, Chesco, Bejos, Isco, Kabastone, Harmodancer,R Kelly, Imma name, Redock Mauzo na Muu Bella ambaye mdogo wake Eneck Bella wa Yamoto Bendi

Marapa kuna Totoo Kalala na Sindano, na pia safu ya unenguaji yupo Mkongwe Queen Suzy na Iniesta.

Advertisement