Shikalo arudishwa kikosi cha kwanza

KIPA namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo amerudishwa kikosi cha kwanza leo Jumamosi dhidi ya Prisons baada ya kukalishwa benchi kwenye michezo sita ya Ligi Kuu Bara.
Yanga inatarajia kuwa mwenyeji wa Prisons kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 1usiku.
Kwa mujibu wa kikosi kilichotolewa na benchi la ufundi la timu hiyo Shikalo anaanza na Juma Abdul, Adeyum Saleh, Lamine More, Ally Mtoni, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa, Yiype Gislain, Tariq Seif na Benard Morrison.
Shikalo mara ya mwisho kucheza kikosi cha kwanza ni mchezo wa ligi kati ya Yanga na Azam FC ambapo mchezo ulimalizika kwa timu hiyo kukubali kipigo cha bao 1-0 bao lililofungwa na Ally Mtoni.
Tangu hapo hajacheza michezo sita ambayo ni dhidi ya Singida United,  Prisons, Mtibwa Sugar, Lipuli FC,  Ruvu Shooting, Mbeya City na leo ndio amepata nafasi ya kukaa golini mchezo dhidi ya Prisons.