Shiboub apata dili jipya Algeria

Muktasari:

Shiboub amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo ya Algeria kwa mkataba wa miaka miwili.


ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Sharaf Shiboub amejiunga na klabu ya Cs Constantine inayoshiriki Ligi kuu nchini Algeria kwa mkataba wa miaka miwili.

Kupitia kwa wakala wake anayefahamika kwa jina la Sifezasports, aliweka katika ukurasa wake kwamba mteja wake huyo amejiunga na klabu hiyo yenye mtaji wa mashabiki katika ligi ya Algeria.

"Mteja wetu amekubaliana kujiunga Cs Constatine na hii ni klabu kubwa yenye mtaji wa mashabiki katika ligi ya Algeria".

Shiboub raia wa Sudan alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea katika klabu ya Al Hillal ya nyumbani kwao.

Baada ya kumaliza mkataba, kiungo huyo hakuongezewa mkataba huku kukiwa na tetesi nyingi za mchezaji huyo kuhusishwa kutimkia Yanga.

Mwishoni mwa msimu uliopita, Shiboub alikosa namba katika kikosi cha kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck.