Shearer ampa tano Solskjaer

Muktasari:

  • Licha ya kufungwa na Paris Saint-Germain wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Solskjaer ameshinda mechi 11 kati ya 13.

London, England. Nguli wa zamani wa England, Alan Shearer amesifu kazi nzuri ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Shearer amesema kocha huyo wa muda amekuwa katika ubora wake na ameiweka Manchester United katika nafasi bora.

Kocha huyo alisema Man United imerejea katika mstari baada ya kufanya vyema katika mechi zake tangu alipotwaa mikoba ya Jose Mourinho.

Kauli ya nahodha huyo wa zamani wa England, imekuja muda mfupi baada ya Man United kuilaza Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA juzi usiku.

Licha ya kufungwa na Paris Saint-Germain wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Solskjaer ameshinda mechi 11 kati ya 13.

“Ni rahisi kutamka amefanya kazi nzuri sana, amerejesha timu katika mstari,”alisema Shearer aliyewahi kuinoa Newcastle United.

Pia nyota wa zamani wa timu hiyo, Phil Neville alisema uamuzi wa Solskjaer kumpanga Herrera umekuwa na mafikio katika mchezo wa juzi. “Alicheza kwa kiwango bora, ameshambulia. Ni mchezaji hodari lakini hakufanya vizuri akiwa chini ya Jose Mourinho,” alisema Neville ambaye pia ni kocha.