Sh10 milioni tu kuibeba AFC

Saturday February 15 2020

 UONGOZI wa AFC,Ligi Kuu Bara,Gwambina FC,Ligi Kuu,Pamba FC,

 

By Mussa Juma,Arusha

UONGOZI wa AFC ya jijini hapa, umesema unahitaji Sh10 milioni tu timu yao kupanda Ligi Kuu Bara ambapo wadau wa soka wanahitaji kusaidia kupatikana kwa fedha hizo.

Msemaji wa klabu hiyo, Bahati Msilu ameliambia Mwanaspoti kuwa timu yao yenye alama 23 imebakiza michezo minane kumaliza ligi hiyo ambapo wao wanashika nafasi ya tatu kundi B na kwamba, uhakika wa kupanda upo. “Kati ya michezo hiyo minane, mitatu tutacheza nyumbani na mitano ugenini, hivyo tukipata Sh10 milioni kwa ajili ya kambi na usafiri wa uhakika tuna uhakika wa kushinda michezo yote na kupanda daraja,” alisema.

“Tunaomba wakazi wa Arusha na mikoa mingine ambao ni marafiki wa AFC waendelee kutupa ushirikiano ili kuhakikisha inarudi Ligi Kuu na kutoa upinzani kwa timu kongwe kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.” Katika kundi B, timu ambayo inaongoza hadi jana ni Gwambina FC ya Misungwi, Mwanza yenye alama 28 ikifuatiwa na Geita Gold yenye alama 25 huku timu inayoburuza mkia kundi hilo lenye timu 12 ni Pamba FC.

Advertisement