Serikali: Mashabiki Simba, Yanga wametufunza, fainali tutapunguza zaidi

Tuesday July 14 2020

 

By Imani Makongoro

SERIKALI imesema changamoto ya kupeana nafasi kwa mashabiki walioingia uwanjani katika mchezo wa Simba na Yanga inaashiria elimu zaidi inahitaji ili kuchukua tahadhari ya janga la maambukizi ya virusi vya corona viwanjani.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, Serikali iliruhusu mashabiki 30,000 kati ya 60,000 wanaojaza Uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo huo 'live', kwa lengo la mashabiki kuachiana nafasi ili kuchukua tahadhari ya corona.

Hata hivyo ilikuwa tofauti, kwani licha ya baadhi ya majukwaa kuwa tupu, lakini mashabiki waliendelea na utamaduni waliouzoea wa kukaa karibu karibu uwanjani na kutoachiana nafasi.

"Imekuwa changamoto sana, bahati mbaya mashabiki wetu wamezoea kukaa pamoja, lakini wanahitaji elimu zaidi kipindi hiki cha tahadhari," amesema.

Amesema mchezo huo umewafundisha kuweka mkazo katika kuchukua tahadhari na kuongeza kuwa katika mechi ya fainali ya kombe hilo ambayo itachezwa mjini Sumbawanga kuna uwezekano idadi ya mashabiki watakaoingia uwanjani ikapunguzwa zaidi.

Uwanja huo Nelson Mandela una uwezo wa kuingiza mashabiki.

Advertisement

''Simba na Yanga tuliweka idadi ya nusu mashabiki, lakini haikusaidia, kwenye fainali hiyo (Simba vs Namungo) kuna uwezekano hata hiyo ya nusu mashabiki ikapunguzwa zaidi," amesema.

Amesema watafanya tathimini ya mechi ya Simba na Yanga, kabla ya kuja na mkakati wa nini watafanya.

Kuhusu sabuni za kunawia mikono kukosekana katika mchezo huo, Singo amesema idadi ya zilizokuwepo zilizidiwa na wingi wa mashabiki.

"Wakati milango ya uwanja inafunguliwa, sabuni zilikuwepo, itakuwa ziliisha baadae, japo hiyo pia ni changamoto ambayo tutaijadili wakati wa tathimini," amesema.

Advertisement