Serengeti Boys kujiandaa mechi za kimataifa Afcon

Muktasari:

Waziri amesema kwa sasa vijana hao wanaelekea Arusha ambako watacheza michezo kadhaa kabla ya Machi 3 kuelekea Gine kwa mwaliko wa UEFA.

Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametaja baadhi ya maandalizi ya timu ya vijana ya Serengeti Boys kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON.

Dk Mwakyembe amesema hadi sasa timu hiyo iko kambini kwa wiki ya tatu na jana iliichama Azam Fc ya chini ya miaka 20 kwa mabao 5-0.

Waziri amesema kwa sasa vijana hao wanaelekea Arusha ambako watacheza michezo kadhaa kabla ya Machi 3 kuelekea Gine kwa mwaliko wa UEFA.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto aliyetaka kujua ni maandalizi gani yanayofanyika kwa timu hiyo ili kombe libaki nchini kama alivyosema jana Waziri Mkuu.

"Huko Gine tutacheza na Australia, Uturuki na wenyeji na mashindano hayo yatakwisha Machi 11 kisha watapita Hispani na kisha Cameroon na huko kote watacheza kabla ya kupita Ruanda kisha watarudi kwa mechi yabufunguzi