Sarri apiga hesabu za kuibomoa Napoli

Friday October 12 2018

 

London, England. Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amejipambanua kuwa ni mmoja wa makocha bora duniani, baada ya kuleta mapinduzi ya haraka, amepanga kuanza kuimarisha kikosi chake.

Sarri aliyetua Stamford Bridge, wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi akitokea Napoli ya Italia, alitumia muda mchache kukijenga kikosi akiwatumia wachezaji wale wale aliowakuta na kuongeza wachache.

Wachezaji aliowanunua Sarri baada ya kutua Chelsea ni makipa wawili, Kepa Arrizabalaga na Rob Green, na viungo Mateo Kovavic na Jorignho.

Katika dirisha la usajili la Januari, kocha Sarri amepanga kuongeza vifaa vingine na moja ya wachezaji wanaotajwa zaidi ni beki wa Napoli, Elseid Hysaj raia wa Albania.

Sarri anaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na bodi ya Chelsea akiwemo Mtendaji Mkuu Marina Granovskaia pamoja na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich.

Kocha huyo Mtaliano amekuwa mkimya kuzungumzia usajili na pia ameonekana kujua kubana matumizi asiyependa kugombea kwani kati ya wachezaji wanne aliowasajili klabuni hapo wawili aliwasajiliwa kwa dau dogo kwa kuwa walikuwa wachezaji huru.

Advertisement