Sarpong nje, Yacouba ndani

Kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic amefanya badiliko moja katika kikosi chake akimuacha nje mshambuliaji wake Michael Sarpong huku akimuanzisha Yacouba Sogne.

Yanga inashuka masaa machache baadaye nyumbani wakiwakaribisha Coastal Union ambapo Krmpotic ameeendelea kuuamini ukuta wake uleule ambao haujaruhusu bao katika mechi tatu zilizopita.

Kwenye ulinzi ameanza na kipa Metacha Mnata, kulia akiwa Kibwana Shomari kushoto akiwa Yassin Mustapha huku mabeki wa kati wakiendelea Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.

Kwenye safu ya kiungo nako hakuna mabadiliko makubwa ambapo Feisal Salum,Zawadi Mauya na Mukoko Tonombe wameendelea kuongoza eneo hilo.

Kikosi hicho ambacho kinaonekana kitatumia mfumo wa 4-3-3 katika safu ya mbele kitakuwa na Carlos Guimaraes 'Carlinhos sambamba na Yacouba na winga Tuisila Kisinda.

Kwenye benchi wapo kipa Farouk Shikhalo mabeki Adeyun Saleh, Said Juma viungo Abdulaziz Makame, Deuse Kaseke, Haruna Niyonzima na mshambuliaji Ditram Nchimbi