Sancho amtoa mafichoni Wenger

Muktasari:

Wenger ambaye aliondoka msimu uliopita baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 22, alisema alitaka kumnasa kinda huyo wakati akijiandaa kutimka kwenye klabu yake ya utotoni, Manchester City.

London, England. Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua siri alikuwa katika nafasi nzuri ya kumnasa winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho alipokuwa akiwanoa bunduki hao wa London.

Wenger ambaye aliondoka msimu uliopita baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka 22, alisema alitaka kumnasa kinda huyo wakati akijiandaa kutimka kwenye klabu yake ya utotoni, Manchester City.

“Nilimwona ni mchezaji mzuri lakini hakuwa na nafasi ya kucheza, kuna mambo yalitokea sikufanikiwa kukamilisha usajili wake,” alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Monaco ya Ufaransa.