Sanchez mtampenda msimu ujao hapo Manchester United

Tuesday May 21 2019

 

Manchester, England.Nyota Alexis Sanchez amepanga kukatisha likizo yake na kurudi mazoezi mapema ili kujiweka fiti asije akafunguliwa mpango wa kutokea Manchester United mapema bila ya kufanya mambo makubwa kwenye kikosi hicho.

Sanchez amekiri kuteswa na kiwango chake kibovu tangu alipotua Man United na mwishoni mwa msimu aliwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo akidai kwamba majeruhi yamemwangusha na kutibua mipango yake.

Staa huyo wa zamani wa Arsenal amefunga mara moja tu kwenye Ligi Kuu England msimu uliomalizika hivi karibuni na hivyo anataka kuanza mazoezi mapema sana ili kujiweka fiti akirudi msimu ujao aje kuwashika.

Alikuwa akiwekwa benchi tu chini ya Jose Mourinho kabla ya kuja kukutana na wakati mgumu tena mbele ya kocha mpya Ole Gunnar Solskjaer.

Kulikuwa na taarifa kwamba beki huyo angeondoka Old Trafford katika dirisha hili la majira ya kiangazi ili kuondokana na majanga ya soka la England.

Sanchez kwa sasa amerudi kwao Chile kusalimia familia na marafiki zake, mahali ambako atakuwa bize kufanya mazoezi ili kujiweka sana huku akitaka kurudi Carrington mapema zaidi kabla ya Julai 2, ambapo mastaa wengi wa Man United wameamua wawasili mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Advertisement

Sanchez amepanga kurudi mwishoni mwa Juni akianza kuingia kwenye mazoezi ya gym kujiweka fiti, Huko kwenye kikosi cha Man United, Sanchez analipwa Pauni 505,000 kwa wiki, lakini sasa anasakwa na Juventus na Inter Milan.

Advertisement