Sanchez ahamishia akili yote Real Madrid

Muktasari:

  • Sanchez aliachwa kwenye kikosi cha United kilichopigwa  mabao 3-1 na Manchester City Jumapili iliyopita kipigo kilichomkera Jose Mourinho.

Manchester, England.  MSHAMBULIAJI wa Manchester United aliyesajiliwa kwa mbwembwe kutoka Arsenal, Alexis Sanchez, ameliamsha upya kabisa, kasema haitaki klabu yake hiyo.

Hatua hiyo ni baada ya kumwambia wakala wake amtafutie klabu nyingine na wakala wake amemwambia kuwa kwa sasa anawasliana na Real Madrid inayoshiriki La Liga.

Mchezaji huyo amekuwa akipambana kupata namba katika kikosi hicho cha Old Trafford na pamoja na kuvuta pesa ndefu, amefunga mabao manne tu katika mechi 29.

Inarripotiwa kuwa Sanchez hana furaha United na mpango wake mzima ni kuondoka Old Trafford na ikiwezekana anataka ifikapo Januari dirisha dogo ltakapofunguliwa.

Mshambuluiaji huyo wa Chile pia amekuwa akitajwatajwa huko Paris Saint-Germain lakini iliwekwa sharti kwamba atachukuliwa ikiwa tu mchezaji mmojawapo kati ya Neymar au Kylian Mbappe wataondoka klabuni.

Lakini kwa mujibu wa televisheni ya Hispania, El Chiringuito, Sanchez amemwambia wakala wake, Fernando Felicevich kumtafutia  timu.

Ripoti zinasema kuwa Felicevich alikuwa akihangaika na kuona uwezekano wa mteja wake kutua Santiago Bernabeu mapema Januari dirisha dogo litakapofunguliwa.

Mabingwa hao wa zamani Hispania wanahangaika kutengeneza safu ya ushambuliaji na ndio maana wamemsajili Mariano aweze kutua Lyon.

Sanchez anaweza kuwa mmoja wa wachezaji mahiri Madrid kwa kuwa ana uwezo wa kucheza pembeni na kati safu ya ushambuliaji.