Samatta, Msuva wakomaa

Sunday September 9 2018

 

By THOMAS NG’ITU

MASHABIKI wa soka nchini jana walisuuzika kwa soka tamu ambalo timu yao ya taifa, Taifa Stars ililolipiga pale Kampala wakati wakiwabana wenyeji wao Uganda na kutoka nao suluhu.

Stars ikicheza kwa mara ya kwanza chini ya Kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike waliwakimbiza wenyeji wao, huku kipa Aishi Manula akifanya kazi kubwa kuokoa michomo ya Waganda hao.

Mechi hiyo ya Kundi L ya kuwania fainali za Afcon 2019 zitakachezwa Cameroon, ilichezwa katika Uwanja wa Namboole ulioharibiwa na maji ya mvua na kuifanya isiwe ya kuvutia hasa kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Stars ilionyesha mabadiliko licha ya kukaa kwa muda mfupi chini ya Mnaigeria, huku mabeki wakionyesha ukomavu na kuwabana washambuliaji wao.

Katika mchezo huo Mbwana Samatta katika dakika 70 alikosa bao la wazi baada ya kumchambua kipa Denis Onyango, lakini hesabu zake zilikataa baada ya kurejesha mpira nyuma na kuokolewa.

Matokeo hayo yanaifanya Uganda kusalia kileleni na alama nne, huku Stars ikichupa hadi nafasi ya pili na alama mbili. Mechi nyingine ya kundi hilo ni Lesotho dhidi ya Cape Verde leo.

Advertisement