Salah tatizo kazidi uchoyo - Wenger

Muktasari:

Katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Liverpool waliupata dhidi ya Burnley, Salah alipondwa baada ya kushindwa kumpasia Sadio Mane kipindi cha pili pindi ambapo mchezaji huyo alipokuwa kwenye eneo zuri zaidi la kufunga.

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema nyota wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah anaweza kuwa bora kama Lionel Messi lakini anatakiwa kupunguza uchoyo.

Wenger ambaye alikuwa akiripotiwa kwamba yuko mbioni kurejea kwenye majukumu yake ya ukocha, anaamini Salah ana uwezo wa kufananishwa na Messi, lakini kuna vitu vichache anatakiwa kuvifanyia kazi.

Kocha huyo, alisema Salah anatakiwa kutofautisha muda ambao anapaswa kulazimisha kufunga na ule ambao atalazimisha kuingia kwenye ngome ya wapinzani kwa lengo la kutoa usaidizi kwa mchezaji ambaye yupo kwenye eneo zuri zaidi.

“Ana uwezo mzuri wa kufunga. Navutiwa na uwezo wake kwa sababu ni mchezaji mzuri, anatakiwa kulifanyia kazi suala la kucheza kitimu kwa kutoa ‘asisti’ muda mwingine kwa wengine,” alisema Wenger.

Katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Liverpool waliupata dhidi ya Burnley, Salah alipondwa baada ya kushindwa kumpasia Sadio Mane kipindi cha pili pindi ambapo mchezaji huyo alipokuwa kwenye eneo zuri zaidi la kufunga.

Mane alionyesha wazi kukerwa na kitendo cha Salah kumnyima pasi.

Roberto Firmino ambaye naye amekuwa akicheza katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool naye amekuwa akitajwa kuwa na tabia ya uchoyo licha ya uwezo mkubwa walionao kwenye umaliziaji.

“Nilikuwa nikipenda vile ambavyo Luis Suarez alikuwa akifan ya kwa Messi na Neymar. Jamaa walikuwa wakifanya kazi pamoja kama timu, il;ikuwa rahisi kila mmoja kung’ara,” alisema.

Mane na Salah wote walimaliza msimu uliopita wakiwa wafungaji bora pamoja na straika wa Arsenal, Pierre Americ-Aubameyang wakifunga mabao 22 kila mmoja katika Ligi Kuu ya England.