Salah asema atafia Liverpool

Muktasari:

Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, amesema hana mpango wa kuihama klabu hiyo ya Ligi Kuu England.

London, England. Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Mohamed Salah amesema hana mpango wa kuihama klabu hiyo kama anavyoshauriwa na Gary Neville.

Neville alimtaka Salah kuondoka kwa mabingwa hao wa Ulaya kujiunga na klabu nyingine ili kupata mafanikio katika soka.

Lakini, nahodha huyo wa Misri amemjibua Neville akiwambia ana amani ndani ya moyo wake hapo Liverpool.

“Nina furaha Liveropool, nina furaha na jiji hili na mashabiki wake kwa ujumla,”alisema Salah.

Mchezaji huyo amekuwa kinara wa mabao Liverpool na miaka miwili iliyopita, alitwaa tuzo ya mfungaji bora.

Katika kuthibitisha ubora wake, Salah alifunga bao katika mchezo dhidi ya Norwich City msimu huu.

Salah amekuwa mfalme wa mabao Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Anfield akitokea AS Roma mwaka 2017.

Neville ambaye ni kocha na mchambuzi, alimtaka nyota huyo kuondoka Liverpool baada ya kuibuka tetesi za kutakiwa na Real Madrid ya Hispania.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27, amefunga jumla ya mabao 55 katika mechi 76 alizocheza Liverpool.