Sakata la Mo, Manara akamatwa

Friday October 12 2018

 

Dar es Salaam. Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amekamatwa na kuwekwa kizuizini kutokana na sakata la kutekwa kwa Mohammed Dewji.

Akithibitisha kukamatwa kwa Manara kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema Manara anashikiliwa kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia, lakini sio kweli

“Manara tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi yeye amekuwa akisambaza taarifa mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ametumwa na familia, lakini sio kweli, hajatumwa na familia hivyo tunamshikilia,” alisema Kamanda Mambosasa.

Mapema jana Manara alinukuliwa akiwataka akisema taarifa ya MO kupata matatizo imemshtua kila mmoja na kwamba bado wanaliachia jeshi la polisi kufanya kazi ya kumpata mwekezaji wao.

“Wanasimba wawe watulivu wakiliachia jeshi la polisi kufanya kazi yake na kwamba wanaamini MO atapatikana akiwa hai,” alisema Manara.

 

Advertisement