Saha amkingia kifua Sanchez Manchester United

Tuesday August 13 2019

 

By Thomas Ng'itu

London. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Louis Saha ameweka wazi bado ana imani kubwa na mshambuliaji wa klabu hiyo, Alex Sanchez.

Saha anaamini licha ya mchezaji huyo kupitia magumu ndani ya miezi 18, msimu huu ataisadia klabu yake kuweza kumaliza katika nafasi nzuri.

"Sanchez hakuwa katika kiwango kizuri msimu uliopita lakini hiyo tayari ni historia, akirejea katika kiwango chake anaweza kuipeleka Utd katika nafasi nne za juu," alisema.

Aliongeza kuanza kwa pamoja na wenzake katika maandalizi ya msimu mpya, hilo litachangia kabisa kuhakikisha anakuwa bora.

"Solskjaer ni mtu ambaye anajua kudili na wachezaji au mtu yoyote yule, sasa anapokuwa yupo na wachezaji wote mwanzoni mwa msimu kila kitu kinaakuwa sawa," alisema.

 

Advertisement

Advertisement