SIRI NJE: City ilitaka kufanya kufuru kwa Messi

Thursday December 7 2017

 

MANCHESTER , ENGLAND. UTATA umezuka na hauwezi kupita hivihivi. Siri imeibuka kwamba kabla ya staa wa Barcelona, Lionel Messi kusaini mkataba mpya na wababe hao wa Nou Camp wiki iliyopita, tajiri wa Manchester City, Sheikh Mansour alipambana kufa na kupona kuinasa saini yake.

Inadaiwa Sheikh Mansour aliweka mezani kiasi cha Euro 100 milioni kama ofa ya Messi mwenyewe kwa ajili ya kusaini kwao, huku akiahidi kumpa mshahara wa Euro 50 milioni kwa mwaka na hivyo kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwa mbali zaidi.

Dau hilo ni sawa na mshahara wa Pauni 850,000 kwa wiki huku bonasi yake ya Euro 100 milioni ikiwa ni sawa na dau la Pauni 85 milioni kama kilainishi cha moyo wa Messi ambaye ameichezea Barcelona tangu akiwa na umri wa miaka 13.

Inadaiwa kuwa tajiri Mansour aliamua kulifanya suala hilo kuwa lake binafsi bila ya kumhusisha mtu yeyote yule na ofa hiyo ilimvuruga Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu ambaye alijua kwamba ingawa Messi alikuwa anataka kubakia Barcelona lakini wangelazimika kufikia dau la City kwa ajili ya kumbakisha.

Inadaiwa Sheikh Mansour hakutaka hata kuutumia urafiki wa kocha wake, Pep Guardiola na Messi kwa ajili ya kumnasa staa huyo wa Argentina kwa sababu hiyo ilikuwa ndoto yake binafsi kumnasa Messi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kwenda City.

Hata hivyo, Barcelona ilifanikiwa kumshawishi Messi kusaini mkataba mpya huku ikihofia kwa kiasi kikubwa kumpoteza staa huyo katika dirisha la Januari ukizingiatia kuwa tayari Barcelona ilikuwa imepata pigo la kumpoteza Neymar kwenda PSG katika dirisha kubwa lililopita. Messi amesaini mkataba ambao kwa sasa utamuona akichukua kiasi cha Pauni 500,000 kwa wiki huku akiwa amepewa kiasi cha Pauni 80 milioni kama bonasi kwa kusaini mkataba huo ambao unatarajiwa kumalizika mwaka 2012 ambapo atakuwa na umri wa miaka 35.

Klabu yoyote ambayo itamtaka Messi italazimika kulipa kiasi cha Pauni 626 milioni kwa mujibu wa kipengele cha mkataba wa Messi kwa sasa na hii inahitimisha ndoto za City kumnasa staa huyo ambaye ilikuwa na ndoto za kumuunganisha na Guardiola.

Katika mkataba wake wa sasa Barcelona ilijadiliana na Messi katika maeneo matatu ambayo ni haki za matumizi ya sura yake, pesa za kupelekwa katika mfuko wake (Lionel Messi foundation) pamoja na mshahara wake halisi mpaka mwaka 2021. Hata hivyo, wakati uvumi kuhusu dili la City na Messi ukiwa unaendelea kuwa gumzo katika vyombo vya habari vya Hispania, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola juzi alitumia mkutano wake na vyombo vya habari kabla ya pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk jijini Kharkiv kukanusha habari hizo.

Alipoulizwa kuhusu ofa hiyo ya City Guardiola alijibu “Lionel Messi amesaini mkataba wiki moja iliyopita. Hili lisingeweza kutokea. Messi alianza maisha yake ya soka pale na atakwenda kumaliza pale. Kama angekuwa anataka kuondoka asingesaini.”

Alipobanwa zaidi na kuambiwa kwamba ofa hiyo ilikwenda kwa Messi kabla hajasaini mkataba mpya, Guardiola ambaye alimfundisha Messi kwa mafanikio Nou Camp alijibu kwa mkato