Ruby azua gumzo ndani ya Wasafi WBC

Muktasari:

Hawa ni baadhi ya wasanii waliosajiliwa katika Lebo ya WCB, Hamornize, Rayvanny, Mboso, Queen Darling, Lavalava.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa amemsainisha msanii kwenye kundi la WCB na kusema watu wabashiri, mashabiki wengi wa muziki wamemtaja msanii nyota wa muziki wa bongofleva, Ruby.

Ruby jina lake halisi Hellen George anasifika kwa sauti yake nzuri na uwezo wa kutumbuiza jukwaani akiwa na nyimbo kadhaa zinazotamba kwa sasa ‘Yule’ Ntande, Alele na nyingine nyingi.

 MCLDigital Julai 15, 2019 ilitinga katika ofisi za WCB na kumkuta Ruby na kumuuliza kulikoni ndio yeye msanii aliyetangazwa na Diamond kuwa amesainiwa na watu wabashiri?

Ruby aliijibu “Hahaha hapana bwana mie nimekuja hapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya Tamasha la Wasafi Festival na sio hicho unachoniuliza dada yangu”

Hata hivyo katika pitapita zetu mitandaoni tulipata kuona picha kibao tu kwenye account ya Ruby alizopiga akiwa kwenye anga za ofisi za Wasafi Classic.

Ruby aliachia picha kadha wa kadha akiwa katika ofisi ya WCB na vilevile akiwa na Diamond Plutnumz.

Wanamuziki waliopo katika lebo ya WCB ni Hamornize, Rayvanny, Mbosso, Queen Darleen, Lavalava.