Royal mzuka kama wote FA Cup

Friday November 8 2019

By Bertha Ismail, Arusha

TIMU ya Watoto wa Kitaa, Royal FC ya jijini hapa wameapa kuiondoa Red Star ya Manyara katika hatua za awali za michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) maarufu kama Kombe la FA.
Royal inakaribishwa na Red Star  kwenye Uwanja wa Kiteto katika michuano hiyo inayoanza rasmi kesho Jumamosi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Michuano hiyo inayoanza na timu za mabingwa wa mikoa na ligi daraja la pili, itachezwa kwa hatua ya mtoano ambapo Royal wamesema kuwa wamejipanga kuvuka kiunzi hicho cha awali.
Katibu wa Royal, Juma Luke alisema wanataka kuwa mkombozi wa soka la Arusha, hivyo kwa kuanzia wataonyesha nguvu yao katika michuano hiyo ya FA.
"Kabla ya msimu wa ligi ya mkoa tulifanya maandalizi ya kutosha kutwaa ubingwa na tumefanikiwa na malengo yetu ni kupanda ligi daraja la pili kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa baadae hivyo kwa kuonyesha  wadau tumedhamiri tutaonyesha nguvu yetu kwenye michuano ya FA," alisema Luke.
Alisema kuwa wanatarajia kufanya usajili wa maana katika dirisha la usajili ili kupata kikosi bora cha ushindani zaidi ya kilivyo sasa.
"Kikubwa tuombe sapoti ya wadau wa soka Arusha katika harakati zetu hizi tufanikiwe, maana heshima tunayosaka niya mkoa, hivyo tunaamini tukiunganisha nguvu mafanikio yapo"

Advertisement