Ronaldo anazeeka na utamu wake

Turin, Italia. Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya ufungaji kwa bao safi la kichwa lililomfanya kwenda hewani mithili ya mcheza kikapu wa zamani wa Marekani, Michael Jordan.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus mwenye miaka 35, alifunga kwa kutumia mtindo wake maarufu wa kupiga vichwa hewani, akienda hewani zaidi katika mchezo dhidi ya Roma juzi usiku.

Ronaldo aliachwa bila kukabwa ndani ya eneo la hatari dakika ya 69, wakati wa mchezo wa Serie A, wakati Juve ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Olimpico.

Krosi ya Danilo kutoka upande wa kulia ilimkuta Ronaldo, ambaye alipiga kichwa kilichokwenda kambani kwa mtindo wa aina yake, akifikisha mabao 450 katika ligi kubwa tano za Ulaya.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, Ronaldo, ambaye alifunga mabao yote mawili katika sare ya 2-2, anakuwa mchezaji wa kwanza kufikia rekodi hiyo katika ligi.

Lakini inaonekana kuwa mashabiki wanazidi kufurahia ubora wake licha ya kuwa ndiyo anaelekea mwisho wa maisha yake ya soka la ushindani.

Katika video ya tuki hilo la bao, mmoja wa mashabiki wake aliandika: “Mtu mwenye miaka 35. Anaruka kama Michael Jordan. Ni ajabu.”

Mmoja wa mashabiki hao pia akikafannisha kicha alichopiga dhidi ya Roma kama ambacho alipiga wakati akiitumikia Manchester United kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2008. Shabiki huyo aliandika: “Same Cristiano Ronaldo. hajaongezeka umri tangu alipofunga kiajabu kwa kichwa dhidi ya Roma.”