Ronaldo amchumbia Georgina Rodriguez

Muktasari:

  • Tangu alipoanza kutoka kimapenzi na Georgina, wamekuwa wakiishi pamoja kama mke na mume na CR7 kaonekana kupunguza makeke yake ya michepuko.

HATIMAYE staa Cristiano Ronaldo kaamua kutulia kabisa baada ya kuripotiwa kamchumbia mpenzi wake Georgina Rodriguez.

Imedaiwa wawili hao siku za hivi karibuni wamekuwa kwenye mishemishe ya kusaka kanisa litakalotumika kufungaia ndoa yao kule Italia.

Hii ni baada yao kunaswa na kamera za mapaparazi mjini Turin, wakiondoka katika Kanisa la Gran Madre ambako wanasemekana walikwenda kufahamu utaratibu unaotakiwa kufuata wakati wachumba wanapotaka kufungia ndoa humo.

Tangu alipoanza kutoka kimapenzi na Georgina, wamekuwa wakiishi pamoja kama mke na mume na CR7 kaonekana kupunguza makeke yake ya michepuko.

CR7 alikutana na Georgina miaka miwili iliyopita jijini Madrid, kichuna huyo alipokuwa akifanya kazi kwenye duka la Gucci.