Ronaldo, Modric, Messi ndani tuzo Ballon d’Or

Muktasari:

Kati ya mwaka 2010 na 2015 Tuzo hizo zilichukuliwa na Fifa na kuitwa Fifa Ballon d'Or, lakini kuanzia mwaka 2016, Fifa ikaanzisha tuzo zake za mwanasoka bora wa mwaka ‘The Best Fifa Football Awards’ na kulirudishia Jarida hilo tuzo za Ballon d'Or.

Paris, Ufaransa. Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Luka Modric na Mohamed Salah ni miongoni mwa wachezaji 30, walioingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya Ballon d'Or

Katika orodha hiyo ya wachezaji 30, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Real Madrid wametawala kwa kutoa wachezaji nane.

Ligi Kuu England imeingiza wachezaji 11 katika orodha hiyo wakiwemo nyota wa Chelsea, Eden Hazard, mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne pia mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane.

Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero pamoja na kipa wa Liverpool Alisson na washambuliaji Sadio Mane na Roberto Firmino.

Kiungo Paul Pogba wa Manchester United, kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante na kipa Tottenham, Hugo Lloris wote wamechaguliwa.

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Juventus akitokea Real Madrid msimu huu mwaka jana alishinda Ballon d'Or na kufikia tuzo ya tano sawa na Lionel Messi.

Tuzo ya Ballon d'Or, ilitolewa kwa mara ya kwanza 1956, na imekuwa ikitolewa kila mwaka.

Sherehe za kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu zitafanyika Paris hapo Desemba 3, na kwa mara ya kwanza tuzo hizo kwa mwaka huu zitaelekezwa pia kwa mwanasoka bora wa mwaka mwanamke na majina 15 yametajwa kuwania tuzo hiyo.

Mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora mwanamke wa Fifa mwaka 2018 Marta kutoka Brazil anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ya ‘Women's Ballon d'Or’ atakayechuana na Christine Sinclair, Lieke Martens, Megan Rapinoe wa Marekani na Sam Kerr wa Australia.

Baadhi ya wengine wanowania tuzo hiyo ni, Pernille Harder, Lindsey Horan, Lucy Bronze, Fran Kirby, Ada Hegerberg, Amandine Henry, Saki Kumagai, Dzsenifer Marozsan, Amel Majri na Wendy Renard.

Wanaowania kwa wanaume tuzo ya BALLON D'OR:

Alisson (Liverpool), Sergio Aguero (Manchester City), Gareth Bale (Real Madrid), Karim Benzema (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris Saint-Germain), Thibaut Courtois (Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Juventus), Kevin De Bruyne (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool), Diego Godin (Atletico Madrid) na Antoine Griezmann (Atletico Madrid).

Wengine ni Eden Hazard (Chelsea), Isco (Real Madrid), Harry Kane (Tottenham Hotspur), N'Golo Kante (Chelsea), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Mario Mandzukic (Juventus), Sadio Mane (Liverpool), Marcelo (Real Madrid), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid)

Pia wapo, Neymar (Paris Saint-Germain), Jan Oblak (Atletico Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Ivan Rakitic (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Mohamed Salah (Liverpool), Luis Suarez (Barcelona), na Raphael Varane (Real Madrid).