Rodgers: Corona imenikumbusha Mlima Kilimanjaro

Muktasari:

Kabla ya kuinoa Leicester City, Rodgers aliwahi kuwa kocha wa timu za Celtic, Liverpool, Watford, Reading na Swansea City

 

London. Kocha wa Leicester City, Brendan Rogders amekuwa kocha wa pili kuthibitisha kuuma ugonjwa corona baada ya Mikel Arteta kuumwa Machi mwaka huu.

Rodgers mwenye umri wa miaka 47 amesema tabu kubwa aliyoipata tangu kuumwa ugonjwa huo ni changamoto ya upumuaji.

“Ilikuwa ni vigumu kutembea ikanikumbusha kipindi nilivyopanda Mlima Kilimanjaro kadri unavyopanda ndivyo unavyopata tabu katika kupumua” amesema Rodgers

Rodgers ameeleza “Tulikuwa na mapumziko ya wiki moja ya mapumziko na tulitakiwa kucheza Machi 14 na baada ya ile wiki nikaanza kuumwa”

Kwa muda wa wiki tatu sikuweza kusikia harufu wala ladha. Sikuwa na nguvu na baada ya wiki mke wangu alipata changamoto hizohizo. Tulipima na kukutwa tuna ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona” ameongeza Rodgers

Rodgers alipanda Mlima Kilimanjaro uliopo mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania mwaka 2011 wiki kadhaa baada ya kushinda mechi za mtoano (Championship play-off final) dhidi ya Swansea 

Kocha huyo ameongeza kuwa amefurahi wachezaji kurudi mazoezini kujianda na Ligi inayotarajiwa kuendelea Juni 13.