Riphat ajifunga Mtibwa Sugar

Muktasari:

Kabla ya kutua Mtibwa Sugar, mshambuliaji huyo alikuwa akiichezea Ndanda FC ya mkoani Mtwara aliyoitumikia kwa misimu miwili.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Riphat Khamis (19) ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo wa zamani wa Ndanda FC amesaini mkataba huo mpya katika kipindi ambacho mkataba wake wa awali umebakiza mwaka mmoja kabla ya kumalizika.

Riphat ni mchezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', amekuwa akihaha kusaka nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Mtibwa Sugar tangu aliposajiliwa na timu hiyo mwaka jana.

Uwepo wa washambuliaji Kelvin Sabato, Stamil Mbonde, Haruna Chanongo na Juma Liuzio umemweka Riphat kwenye nafasi ngumu ya kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.