Ridhiwani: Uchaguzi ubadili mfumo huu

Tuesday April 16 2019

MBUNGE wa Chalinze na mwanachama wa klabu ya

MBUNGE wa Chalinze na mwanachama wa klabu ya Yanga, Ridhiwani Kikwete 

By Charity James


MBUNGE wa Chalinze na mwanachama wa klabu ya Yanga, Ridhiwani Kikwete amesema mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo yanakwamishwa na uchaguzi mkuu ambao ulipaswa kufanyika tangu Januari 13 mwaka huu.

Hivi sasa uchaguzi huo umepangwa kufanyika Mei 5 mwaka huu ambapo zaidi ya wagombea 40 wamechukuwa fomu kugombea nafasi mbalimbali.

Ridhiwani aliliambia Mwanaspoti kuwa, ni muda mrefu sasa tangu zoezi la uchaguzi limeanza kupigiwa kelele lakini hakuna cha msingi kilichofanyika na kuwaomba wanachama kwa umoja wao kuhakikisha wanaungana kuhamasishana kufanya uchaguzi wa haki na utulivu ili waweze kuingia kwenye mfumo bora.

Alisema haiwezekani klabu kama Yanga ambayo ina wanachama wengi wakashindwa kuisaidia timu hiyo kuingia katika mfumo wa kujitegemea na kuamua kuingia kwenye migogoro.

“Klabu ili ifanye vizuri inahitaji kuendeshwa kisasa na siyo kumtegemea mtu mmoja kama ilivyo sasa,” alisema Ridhiwani.

Advertisement