Riadha yatumika kupinga ukatili Arusha

Muktasari:

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo Bi. Faustine Nillan anasema mbio hizo na matembezi ya hiayari ni sehemu ya Kanisa ya kuhamasisha jamii kuacha ukatili.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kupitia Kurugenzi wanawake na watoto inaadhimisha kupinga ukatili kwa jamii kwa kufanya riadha ya mbio za kilomita 5 na matembezi ya hiari.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo Bi. Faustine Nillan anasema mbio hizo na matembezi ya hiayari ni sehemu ya Kanisa ya kuhamasisha jamii kuacha ukatili.

Anasema maadhimisho hayo wanatarajia kuyahitimisha Disemba 8 mwaka huu kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Arusha ikiwa ni mahususi kwao kuadhimisha siku 16, za kupinga ukatili wa Kijinsia ambayo huadhimishwa kila mwaka Disemba 25 hadi 10

Mgeni rasmi  ambaye ni Msaidizi wa Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dean Gidion Kivuyo alikabidhi cheti cha ushindi wa nafasi ya kwanza kwa mbizo za riadha kwa wanawake za kilometa tano, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto.

Mbio hizo zimeandaliwa na Kurugenzi ya Wanawake na Watoto ya KKKT Makao Makui.