Rekodi hizi zimemuangusha Amunike Taifa Stars #2

Tuesday July 16 2019

 

WIKi iliyopita tuliangalia namna ‘kipindi cha giza’ kilivyokuwa katika soka la Tanzania na namna ambavyo nchi iliingia kwenye ‘zama za mwangaza’ na rekodi zilizowekwa na makocha waliowahi kuinoa Taifa Stars kabla hata ya kuja kwa Emmanuel Amunike.

Leo tunaendelea pale tulipoishia na kuona kama kutimuliwa kwa Amunike kulikofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuna mashiko ama kaonewa tu Endelea..!

4. DK MSHINDO MSOLLA 2005-2006

Septemba 2005 Dkt Msolla akaajiriwa tena kuwa kocha wa muda wa Taifa Stars wakati TFF ikifanya mchakato wa kumpata kocha mpya wa kigeni.

Katika mechi zake 10 za kwanza, alishinda 6, na kutoka sare 2.

30/07/2006 Tanzania 1-0 Rwanda

Advertisement

30/06/2006 Shelisheli 2-1 Tanzania

26/06/2006 Tanzania 2-1 Mauritius

01/04/2006 Tanzania 2- 2 Zanzibar

06/12/2005 Rwanda 3-1 Tanzania

04/12/2005 Tanzania 1-0 Eritrea

02/12/2005 Tanzania 1-1 Zanzibar

28/11/2005 Tanzania 2-1 Burundi

09/11/2005 Tanzania 1-0 Zanzibar

06/11/2005 Tanzania 1- 0 Zanzibar

5. MARCIO MAXIMO 2006-2010

Mwaka 2006, Tanzania ikapata kocha kutoka Brazil, Marcio Maximo. Katika mechi zake 10 za kwanza, Maximo alishinda 6 na kutoka sare 3.

Kocha huyu ndiye aliyeishauri TFF kuwa na jezi maalumu ya Taifa Stars na alichagua rangi ya bluu. Kisa cha kufanya hivyo ni zomea zomea ya mashabiki wa Simba siku Stars ilipocheza na Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa, sasa Uhuru. Stars walivaa jezi za njano siku hiyo, katika mchezo ambao ulikuwa wa mwisho kwa Dk. Mshindo Msolla na Maximo alikuwa jukwaani akiiangalia timu yake mpya. Kufuatia zomea zomea hoyo, Maximo akasema hataki kuona watu wanagawanyika kwenye kuishangilia timu yao. Akaichagua rangi ambazo hazipo Simba wala Yanga. Akasema hii itakuwa The Blues of Africa. Rekodi yake ilikuwa hivi;

10/12/2006 Tanzaia 2-0 DR Congo

05/12/2006 Tanzania 1-2 Rwanda

01/12/2006 Tanzania 3-0 Djibouti

28/11/2006 Tanzania 2-1 Malawi

25/11/2006 Ethiopia 1-2 Tanzania

18/11/2006 Angola 1-1 Tanzania

08/10/2006 Msumbiji 0-0 Tanzania

30/09/2006 Tanzania 0-0 Kenya

02/09/2006 Tanzania 2-1 Burkina Faso

17/08/2006 Tanzania 1-0 Zanzibar

6. JAN POULSEN

Maximo aliondoka 2010 na nafasi yake kuchukuliwa na Jan Poulsen, kutoka Denmark.

Katika mechi zake 10 za kwanza, Stars ilishinda 4 na kutoka sare 2.

05/01/2011 Misri 5-1 Tanzania

10/12/2010 Tanzania 0-0 Uganda

08/12/2010 Tanzania 1-0 Rwanda

03/12/2010 Tanzania 2-0 Burundi

30/11/2010 Tanzania 3-0 Somalia

27/11/2010 Tanzania 0-1 Zambia

23/11/2010 Tanzania 1-0 Kenya

09/10/2010 Tanzania 0-1 Morocco

03/09/2010 Algeria 1-1 Tanzania

11/08/2010 Tanzania 1-1 Kenya

7. KIM POULSEN

Baada ya ujio wa Jan Poulsen, TFF ilimletea raia mwingine wa Denmark, Kim Poulsen afundishe timu za vijana. Lengo lilikuwa kutengeneza falsafa moja kuanzia kwa vijana hadi timu ya wakubwa.

Mwaka 2012 Jan Poulsen akaondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kim Poulsen.

Rekodi ya kocha huyo ilikuwa kama ifuatavyo;

03/12/2012 Tanzania 2-0 Rwanda

01/12/2012 Tanzania 7-0 Somalia

28/11/2012 Burundi 1-0 Tanzania

25/11/2012 Tanzania 2-0 Sudan

14/11/2012 Tanzania 1-0 Kenya

15/08/2012 Botswana 3-3 Tanzania

17/06/2012 Msumbiji 1-1 Tanzania

10/06/2012 Tanzania 2-1 Gambia

02/06/2012 Ivory Coast 2-0 Tanzania

26/05/2012 Malawi 0-0 Tanzania

8. MART NOOIJ

Mwaka 2013 TFF ilipata uongozi mpya chini Jamal Malinzi. Uongozi huu ukamuondoa Kocha Kim Poulsen ambaye aliletwa na TFF ya Tenga na kumleta ‘chaguo lao’, mdachi Mart Nooij. Wakati anakuja, timu ilikuwa chini ya kocha wa muda mfupi, Salum Mayanga.

Aprili 26, 2014, Nooij (kabla hajakabidhiwa timu) alikuwepo Uwanja wa Taifa, kuiangalia timu yake mpya ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi katika siku ya Muungano, na kupoteza 3-0.

Wakati huo kulikuwa na vuguvugu la serikali tatu, kwa hiyo ukazuka msemo wa kwamba tayari Burundi wametujibia swali letu.

Katika mechi zake 10 za kwanza, mdachi huyu alishinda mechi 3 na kutoka sare 3.

04/05/2014 Tanzania 0-0 Malawi

18/05/2014 Tanzania 1-0 Zimbabwe

27/05/2014 Tanzania 1-0 Malawi

01/06 2014 Zimbabwe 2-2 Tanzania

01/07/2014 Botswana 4-2 Tanzania

20/07/2014 Tanzania 2-2 Zimbanwe

03/08/2014 Zimbabwe 2-1 Tanzania

07/09/2014 Burundi 2-0 Tanzania

12/10/2014 Tanzania 4-1 Benin

16/11/2014 Tanzania 1-1 eSwatini

9. BONIFACE MKWASSA

Safari ya Mart Nooij ikaishia uwanja wa Amaan Zanzibar kwa kipigo cha 3-0 kutoka kwa Uganda, kufuzu CHAN.

Baada ya kushuhudia makocha wengi wa kigeni, ukafika wakati wa wazawa kuchukua timu na zali likamuangukia nahodha wa zamani, Boniface Mkwassa.

Kama ilivyokuwa kwa mabosi wake wa ‘zama za giza’, Dk. Mshindo Msolla na Hafidh Badru, naye alikuwa akirejerea Stars kwa mara nyingine tangu wakati ule.

Mechi zake 10 za kwanza zilishuhudia akishinda 3 na kutoka sare 4.

94/07/2015 Uganda 1-1 Tanzania

28/08/2015 Tanzania 1-2 Libya

05/09/2015 Tanzania 0-0 Nigeria

07/10/2015 Tanzania 2-0 Malawi

11/10/2015 Malawi 1-0 Tanzania

14/11/2015 Tanzania 2-2 Algeria

17/11/2015 Algeria 7-0 Tanzania

22/11/2015 Somalia 0-4 Tanzania

24/11/2015 Rwanda 1-2 Tanzania

28/11/2015 Tanzania 1-1 Ethiopia

10. SALUM MAYANGA

Mwaka 2017 Charles Boniface Mkwassa akaondoka na nafasi yake kuchukuliwa na nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Salum Mayanga alifanya kazi nzuri na ni miongoni mwa makocha wachache waliopata matokeo bora wakiwa na Stars. Katika mechi zake 10 za kwanza, Mayanga alishinda nne na kutoka sare tano

25/03/2017 Tanzania 2-0 Botswana

28/03/2017 Tanzania 2-1 Burundi

10/06/2017 Tanzania 1-1 Lesotho

26/06/2017 Tanzania 2-0 Malawi

27/06/2017 Angola 0-0 Tanzania

29/06/2017 Tanzania 1-1 Mauritius

02/07/2017 Afrika Kusini 0-1 Tanzania

05/07/2017 Zambia 4-2 Tanzania

07/07/2017 Tanzania 0-0 Lesotho

15/07/2017 Tanzania 1-1 Rwanda

Agosti 2018, Mayanga akamuachia timu Emmanuel Amunike, gwiji wa soka la Afrika. Matumaini yalikuwa makubwa kwa Watanzania kwamba uzoefu wake kama mchezaji akichezea klabu kubwa kama Barcelona, ungeweza kuongeza kitu kwenye soka letu, lakini hali imekuwa tofauti kwani matokeo yake hayakuwaridhisha wengi.

Advertisement