Real Madrid yawatolea macho Mbappe, Neymar

Muktasari:

  • Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kuwanasa mastaa mbalimbali majira haya ya kiangazi katika kampeni za kutaka kukiboresha kikosi chao ambacho hakikuwa na msimu mzuri.

Madrid, Hispania. Miamba ya soka la Hispania, Real Madrid inasubiri uamuzi ya nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe au Neymar kuhusu uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

Gazeti maarufu Hispania, AS limechapisha leo (Alhamis) taarifa ya mastaa hao, yenye kichwa cha habari kuwa ni Mbappe au Neymar waliokwenye mtego wa Florentino (Perez).

Taarifa hiyo iliendelea, “Unasubiriwa muongozo wa mmoja wapo au wengine wanaweza kuingia.”

Mbappe ambaye alitwaa tuzo ya mchezo bora wa mwaka wa Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’ maneno yake aliyosema Jumapili, baada ya kutwaa tuzo hiyo, yameanza kutofasiriwa kuwa huenda yuko mbioni kuondoka.

“Kuna mambo ambayo hayakwenda sawa (huu msimu), lakini ndio maisha ya mpira yalivyo, kikubwa tumeweza kuendelea kutetea ubingwa wa Ligi.

“Niseme asante kwa kocha na kwa klabu tena. Kitu muhimu kwangu ni kwamba hii ni hatua ya kwanza au ya pili kupiga kwenye uchezaji wangu soka,” alisema Mbappe.