Real Madrid imefulia yashindwa kusajili

Friday January 12 2018

 

Madrid, Hispania.Rekodi za uhamisho zinavunjwa kila uchwa msimu huu, lakini Real Madrid imekuwa si miongoni mwa klabu kubwa zilizotoa fedha kununua mchezaji yeyote.

Karibu euros 2.4 bilioni tayari zimetumika katika usajili wa klabu 14, lakini Real Madrid wenyewe wametumia kiasi cha euro 42.5 milioni kusajilia.

Ni wazi mambo yamekuwa tofauti sasa kwa rais wa Real, Florentino Perez anayesifika kwa kumwaga fedha katika kusajili Galacticos kama ilivyokuwa kwa Luis Figo, Zinedine Zidane, David Beckham, Ronaldo, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.