Rashford hayumo kikosini Man United ya Anfield

Muktasari:

Manchester United na Liverpool zilimaliza kwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND . STRAIKA, Marcus Rashford hakuwamo kwenye kikosi cha awali cha Manchester United kilichokusanyika kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool huko Anfield usiku Jumapili.
Fowadi huyo alikuwa na hatihati ya kukosa mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyopata kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Wolves katikati ya wiki iliyopita, hakuonekana wakati wachezaji wenzake walipokutana kukamilisha mambo ya mwishomwisho kabla ya kwenda Liverpool.
Wachezaji wa Man United walikutana kwenye hoteli ya Lowry iliyopo jijini Manchester, ambapo alitumia usiku wao wa Jumamosi hapo kujiandaa nna mchezo wao wa Anfield. Wachezaji wote walikuwapo isipokuwa Rashford tu.
Taarifa hizo ni za neema kwa Liverpool, kutokana na ukweli kwamba Rashford amekuwa kwenye kiwango bora akifunga mabao 16 katika mechi 21 alizocheza tangu mara ya mwisho alipowafunga Liverpool katika mchezo uliofanyika Old Trafford, Oktoba mwaka jana.