Rashford awekwa kundini Barcelona

Sunday April 14 2019

 

MANCHESTER
ENGLAND

NAKWAMBIA Ole Gunnar Solskjaer kazi anayo. Shughuli ya kuwabakiza mastaa wake huko Manchester United ni pevu baada ya Barcelona kuripotiwa kutaka kuvamia Old Trafford kwenda kufanya mchakato wa kumchukua mshambuliaji, Marcus Rashford.

Kinachoelezwa ni kwamba Barcelona wameamua kumrudisha Rashford kwenye mipango yao ya kumsajili kwenye dirisha lijalo ili kuongeza makali kwenye fowadi yao waendelee kutamba Hispania na Ulaya kwa ujumla.

Taarifa za kutoka Hispania zinafichua kwamba Barcelona wameamua kuachana na mpango wao wa kumnasa straika wa Eintracht Frankfurt, Luka Jovic na hivyo kuhamishia nguvu zao kwenye usajili wa washambuliaji Rashford na Antoine Griezmann.

Barca imeona sio shida kuanza kusumbuana na Real Madrid na Bayern Munich kwenye usajili wa Jovic, hivyo wameamua kuhamisho nguvu huko Man United kunasa saini ya Rashford huku wakimtaka pia staa wa Atletico Madrid, Griezmann.

Advertisement