Rashford apewa kazi kumvuta Sancho

Muktasari:

Rashford hivi karibuni alimtaka Sancho akajiunge na Man United ili kwenda kutengeneza kombinesheni matata katika katika kikosi hicho cha Old Trafford.
Kwa mujibu wa Evening Standard, Rashford sasa amepewa majukumu na kwamba yupo kwenye hatua nzuri ya kumshawishi staa huyo wa zamani wa Manchester City kwenda kujiunga na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.

MANCHESTER, ENGLAND . MANCHESTER United imempa kazi fowadi wa Marcus Rashford kuhakikisha anafanya kila analoweza kumshawishi Jadon Sancho aende kukipiga Old Trafford msimu ujao.
Man United imekuwa ikimfukuzia winga huyo Mwingereza anayewindwa pia na klabu kibao za huko Ulaya. Staa huyo amekuwa moto huko Borussia Dortmund huku klabu nyingine kama Chelsea zikitajwa kuhitaji pia saini yake.
Rashford hivi karibuni alimtaka Sancho akajiunge na Man United ili kwenda kutengeneza kombinesheni matata katika katika kikosi hicho cha Old Trafford.
Kwa mujibu wa Evening Standard, Rashford sasa amepewa majukumu na kwamba yupo kwenye hatua nzuri ya kumshawishi staa huyo wa zamani wa Manchester City kwenda kujiunga na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer.
Sancho amekuwa kwenye kiwango bora kabia msimu huu huko BVB, akigunga mbao 17 katika mechi 35 pamoja na asisti 19.
Rashford, naye kwa upande wake amekuwa na kiwango kizuri kweye kufunga, akitikisa nyavu mara 19 katika michuano yote, lakini sasa ni majeruhi, akisumbuliwa na maumivu ya mgongo tangu Januari.