Rashford aibua hofu Man United

Muktasari:

‘Tutampima kujua ukubwa wa tatizo lake kabla ya kuamua kama atacheza au vinginevyo. Kwa kweli sikupanga kumtumia, alikuwa na maumivu ya goti au la, lakini alipambana,”alisema Solskjaer.

London, England. Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ana hofu ya kumtumia Marcus Rashford katika mchezo wa Jumapili dhidi ya watani wao wa jadi Liverpool.

Rashford (22), aliumia mgongo katika mchezo wa Kombe la FA ambao Man United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Wolves.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amekuwa tegemeo la Man United akiwa amefunga mabao 22 msimu huu.

‘Tutampima kujua ukubwa wa tatizo lake kabla ya kuamua kama atacheza au vinginevyo. Kwa kweli sikupanga kumtumia, alikuwa na maumivu ya goti au la, lakini alipambana,”alisema Solskjaer.

Kocha huyo alisema amecheza kamari kumpanga Rashford katika mchezo huo, lakini jambo la kufurahisha alichangia matokeo mazuri ya Man United.

Alisema Rashford alicheza kwa ufanisi licha ya kucheza kwa tahadhari akihofia kupata maumivu zaidi kutokana na jeraha alilokuwa nalo awali.

Rashford amecheza mechi 13 kati ya hizo akianza katika michezo 11 na amekuwa chachu ya mafanikio katika kikosi hicho.