Ramos akamatiki La Liga

Sunday July 5 2020

 

Madrid, Hispania. Hadi sasa Real Madrid wamewaacha mabingwa watetezi Barcelona kwa pointi saba wakisaliwa na michezi minne baada ya kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penati na beki Sergio Ramos.

Ramos ameendelea kuandika rekodi ya kuwa mfungaji bora wa La Liga tangu irejee baada ya mapumziko ya ugonjwa wa corona akiwa amefunga mabao 5 hadi sasa yakiwemo mawili muhimu yalioamua matokeo.

Barcelona wamebakiwa na michezo mitano ikiwemo mmoja watakaocheza leo usiku na endapo watashinda itawafanya kupunguza gepu la alama saba hadi nne.

Ramos ameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani hususani katika upigani wa penati ambazo zimekuwa zikiamua matokeo kwa timu hiyo inayonolewa na mkongwe Zinedine Zidane.

Ukiacha na rekodi hiyo Ramos anaandika rekodi ya kuwa beki pekee kwa muongo mmoja kufunga mabao 10 kwa msimu pia amefikisha mabao 96 akiwa na Madrid

Advertisement